Wanawake wenye umri mkubwa wametakiwa kuacha kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na vijana wenye umri mdogo, kwani jambo hilo linawapunguzia heshima katika jamii.
Ushauri
huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima
Kihemba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani
yaliyofanyika eneo la Kituo cha Afya Mlandizi, wilayani
Kibaha mkoani Pwani.
Kihemba,
ambaye kitaaluma ni mwanahabari, alisema kuna ripoti za
kipolisi mkoani Pwani zinazoeleza kuna kinamama ambao tayari
wamevuka umri wa miaka 60 wana uhusiano wa kingono na
vijana wenye umri mdogo, jambo linalowapunguzia heshima
katika jamii.
"Kuna
taarifa kuwa miongoni mwenu kuna kina mama wana tabia
mbaya ya kuwa na wapenzi ambao ni vijana wadogo sana
kiumri. Kweli si kweli?" Aliuliza mkuu huyo wa wilaya na wazee hao ambao kwa idadi walikaribia 300, wakaitikia 'Kweliiiii'.
Baadaye,
Mwandishi alimfuata Kihemba na kumwuliza juu ya ukubwa wa
tatizo hilo mkoani humo ambapo alijibu; "Halijawa
tatizo kubwa sana, lakini kuna wachache walio na tabia
hizo mbaya, ndio maana tunaanza kulidhibiti ili
lisisambae kwa kasi maeneo mengine."
Alisema
tatizo hilo kwa ukubwa lipo miongoni mwa wanaume ambao
wamekuwa wakijihusisha na ndoa za utotoni kwa muda mrefu,
huku likilazimisha wanafunzi wa kike kukatisha masomo yao
kuolewa.
Uchunguzi
uliofanywa miongoni mwa wazee ambao walikuwa wanapata
huduma ya bure ya kupima afya zao kwa msaada wa shirika
lisilo la kiserikali la The Good Samaritan Social Services
umethibitisha ubakaji na ndoa za utotoni ni matatizo
makubwa maeneo ya Mlandizi na viunga vyake.
Mkurugenzi
wa Shirika hilo, Elisha Mwamkinga alisema shirika lake
linajitahidi kuwaelimisha wazee kuishi kwa heshima katika
jamii na kuepuka mambo ya aibu miongoni mwao.
Kwa
ufadhili wa Shirika la HelpAge International, zaidi ya
wazee 300 wa Mlandizi walipima afya zao, na wengi wao
wakapongeza juhudi zinazofanya na shirika hilo katika
kuwapa huduma mbalimbali za kiafya na chakula.



Post a Comment