Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm,
amejigamba kikosi chake ni kipana na kinaweza kupambana kwenye mazingira
tofauti iwe kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania bara au ile ya Kombe
la Shirikisho Afrika wanayoshiriki hivi sasa.
Pluijm ameiambia Kandanda kikosi chake kwa sasa kiko
katika ubora wake kutokana na ufiti waliokuwa nao wachezaji wake ambao
pia wanapenda kupata mafanikio.Mholanzi huyo alisema:“Nina orodha kubwa ya wachezaji wenye uwezo na vipaji vya hali ya juu kwa hiyo ndiyo maana hukuona pengo la Andrey Coutinho tulipomkosa kwa mwezi mmoja na hata sasa tunaelekea kucheza na Etoile Sportive du Sahel tunaweza kumkosa Salum Telela inauma lakini tunaye mtu wakuziba nafasi yake.”
Yanga inaongoza ligi kuu bara ikiwa na pointi 46, inafuatiwa na Azam FC yenye pointi 38 na Simba iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35


Post a Comment