Pamoja
na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo
hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa
wanaume.Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka
kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka
kufunga ndoa kuliko ilivyokwa wanaume. Hilo tunaliona
wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati
wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi. Hata hivyo,
kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi
ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko.
(Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa
kabisa)
1.Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake
wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa)
hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume
ambaye angependa awe mume wake.Wanawake hawa hujiamini
zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu
mwanaume wa kumuoa awe nazo.Vigezo hivyo huwa hata kwa
misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao
hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile,
mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti nzuri
n.k.Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele
kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa
tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume
hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.
2. Kutaka mwanaume tajiri
Kuna
wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa
hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana
pesa nyingi.Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume
mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume ana
uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona
huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule
ambaye anahisi ataishi maisha ya kifahari.Hivyo
hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya
mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha
kama huyo mwanaume kampita sana umri.
3. Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili
ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa
haiwezekani na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule
ambaye unampenda na unaamini anakupenda pia.Wengi
katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa kigezo
kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata kwenye
sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo vya mwanamme awe
vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua
kuolewa.Yeye kikubwa anataka ampate mume ambaye
atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo
mume atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanamke
anaaminimsingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya
yeye na mmewe basi! Hana haraka hadi pale atakapompata
mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.
4. Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)
Kuna
wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga;
wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka ama
mwanaume wa aina ipi wanataka.Akija wa mwenye uwezo
atasemanataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo
atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha
hajitumi kutafuta maendeleo.Akija wa kabila hii, atasema
hapana hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi
ni mtu asiyeisha kutoa kasoro za wale ambao wanajitokeza
kutaka kumuoa.Hatimaye inaweza tokea muda wa kuolewa
ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa
hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena
katika soko.
5. Kujiona ni mzuri sana
Kuna
wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia
uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi
kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huona
hata wote kumtamani.Hata hivyo hapo hapo kuna wale
ambao huwa ni wazuri kawaida –ila kwa mtazamowake
hujiona ni mzuri mno hakuna mfano kama yeye; kitendo
ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya kujiona
yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu
anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana.Kitendo hiki
hukuza nyodo za haliya juu ya mwanamke mwenye mtazamo
huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka kuoa –
anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.
6. Kujiona ana Umri mdogo
Binti
yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa
endapo tu karidhia kuolewa.Wanawake wametofautiana
mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri
wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao
hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.Katika kundi hili
umri kuwa mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na
umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali kuna
mwingine anakuwa na miaka 20 na akajionani mkubwa na
anafaa kuolewa.Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa
na malengo ya kutotaka kuharakisha katika
ndoa.Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini
yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake
kuingia katika ndoa.
7. Maradhi hasa UKIMWIHili kama lilivyo kwa wanaume -
Pamoja
na kuhamasishwa kwingina wataalamu wa maradhi ya
HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa
na mahusiano na hata kuoa na kuwana watoto; bado
haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni
waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama
kuwahi kuwa na mtoto.Wengi sana hukata tamaa na huona ni
kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa
tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni
waathirika; afyahudhoofika zaidi.
8. Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana
na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo
huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na
dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya
tamthilia yawe na kwao pia.Hilo linafanya vigezo
ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali
mwanaume kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi
anatarajia.Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha
ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo
yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya
kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.
9. Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo
huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na
baadhi kama haya:- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea
kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki,
majukumu na mengine mengi.- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii
inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine
mama aliteswa sana), na hata ndugu wakaribu kama vile
kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke
huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na
kuonewa.- Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao
unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo
anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kamamume
kwake anaona kama ni utumwa.
10. Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna
wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia
yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza
kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi.Wengi wa aina
hii ya wanawake huwa ni waoga sana wa kuwa karibu na
mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu baadhi
huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na
uchafu.Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya
kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu
ya kutaka kuolewa.

Post a Comment