Mahakama moja mjini Busia,
imewahukumu washukiwa watatu vifungo vya kati ya miaka saba na kumi na
tano gerezani,baada ya kuwapata na hatia ya kumbaka na kumjeruhi
msichana mmoja, aliyefahamika kama Liz.
Liz inasemekana
alishambuliwa na vijana hao na kubakwa wakati alipokuwa akirejea
nyumbani kutoka kwa mazishi ya babu yake katika eneo la Busia Magharibi
mwa Kenya.
Tukio hilo lilizua mjadala mkali nchini Kenya huku
wanaharakati wa kijamii wakishinikiza serikai kuwachukulia washukiwa hao
hatua kali.
Watatu hao walikuwa wamehukumiwa ''kufyeka nyasi katika kituo cha polisi'' na kuachiliwa huru.
Hata
hivyo msichana huyo alikuwa amepooza kiwiliwili chake kuanzia kiunoni
kufuatia kutupwa katika shimo ilikuficha ushahidi alipata
msaada
baada ya wanaharakati wa kupigania haki za kibiniadamu kuishinikiza
polisi kuchukua hatua dhidi ya polisi waliotoa hukumu hiyo nyepesi dhidi
ya watu hao watatu.


Post a Comment