Featured
Loading...

BABA NAYE LOOOOOOOOO NOMA endelea hapa


“Hivi nitarudi vipi nyumbani leo? Hii si aibu kubwa! Yaani mke wangu amejua kila kitu kuhusu mtoto wake. Niliomba samahani siku zile yakaisha, kaenda Tanga nikamleta tena mjini sasa faida yake ndiyo haya yanayonitokea.
“Mbaya zaidi kuna wakati Mwaija alinishukuru kwa kumpangia chumba, sasa pale mama yake si amesikia kila kitu!” alitafakari Masilinde, akaishiwa nguvu na kuanguka chini kisha akapoteza fahamu.
Mwaija alifanya kazi ya ziada kumzindua mpenzi wake huyo lakini alipozinduka na kutulia kidogo wote wakawa na swali moja ni kwa nini mama Mwaija baada ya kukatiwa simu muda huo hakupiga tena?!
Wakiwa wanafikiria kuhusu hilo, simu ya Mwaija ikaita ikiwa kwenye meza ndogo...
“Hebu angalia ni yeye?” alisema Masilinde...
“Mimi naogopa, angalia wewe,” alisema Mwaija.
Simu iliendelea kuita na kila mmoja akiwa hataki kuangalia nani aliyepiga...
“Angalia Mwaija...”
“Angalia wewe bwana mimi naogopa.”
Mwishowe, Masilinde alijitoa fahamu, akaenda kuangalia...
“Mh! Yeye bwana,” alisema akiwa ameishika simu...
“Mimi sipokei hata iweje! Mama anaweza kuniua hata kwenye simu,” alisema Mwaija huku akitetemeka.
Chumba kilizizima, kila mmoja alikosa amani, alikosa raha! Ilifika mahali wote walikaa kitandani wakiwa wamejiinamia kwa mawazo. Kila mmoja aliwaza la kwake, lakini hakuna aliyemwambia mwenzake alichokuwa akikiwaza...
“Mwaija, mimi nadhani kuanzia leo tuamue moja, tuwe mke na mume au tujiue, kwa kuwa najua mimi na mama yako kurudiana hakupo hata iweje?”
Kabla Mwaija hajajibu, meseji kwenye simu yake iliingia, ikaingia pia kwenye simu ya Masilinde...
“Mh! Hizo meseji atakuwa yeye,” alisema Mwaija. Sasa alianza kujijua kumbe yeye ni bogasi kupita wasichana wote duniani. Kuna akili ilikuwa ikimwambia...
Usilikose chombezo hili wiki ijayo. Maoni ushauri: Piga
+255 655 207 520

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts

Popular Posts

© Copyright Right Vision Blog | Designed By Code Nirvana
Back To Top