Matibabu
Lengo kuu la matibabu ni kufanya figo zisiendelee kuathirika. Mojawapo ya njia bora kabisa za kusaidia hilo ni kudhibiti kiwango cha shinikizo la damu kuwa chini ya 130/80 mmHg.
Zipo dawa husaidia tatizo hili kama vile zile za jamii ya Angiotensin Converting Enzyme inhibitors kwa mfano Captopril pamoja na zile za Angiotensin receptor blockers zimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kushusha shinikizo la damu wakati huo huo kudhibiti kasi ya kuharibika kwa figo kutokana na kisukari.
USHAURI
Wagonjwa wanashauriwa kula lishe yenye kiwango kidogo cha mafuta, matumizi ya dawa za kudhibiti kiasi cha mafuta mwilini na kufanya mazoezi mara kwa mara kama vile kutembea kwa saa mbili na wawe wanakunywa maji kwa wingi kabla na baada ya matembezi kwani husaidia sana kuzuia au kupunguza kasi ya kuathirika kwa figo.
Wanashauriwa kubadilisha aina ya chakula wanachokula, kutumia dawa za kisukari kama inavyoshauriwa na daktari na kuchunguza kiwango chako cha sukari kila mara kwani husaidia kuzuia tatizo hili.


Post a Comment