Featured
Loading...

Nepal earthquake: Death toll passes 1,000

Zaidi ya watu 1000 wamekufa kwa tetemeko la ardhi nchini Nepal.
Tetemeko hilo lililopiga mji wa Kathmandu  na Pokhara na nguvu ya kipimo cha 7.8 magnitude kwa nguvu lilitikisa pia India, Bangladesh, Tibet  na mlima Everest.
Serikali imetangaza hali ya hatari na kuanza kukimbiza misaada maeneo yaliyovurugika vibaya.

Kwa mujibu wa televisheni ya CNN kitovu cha tetemeko kilikuwa maili 50 kutoka mji mkuu wa Nepal wa Kathmandu.
Imeelezwa kuwa majengo mengi ya kihistoria mjini Kathmandu yameharibiwa na mpaka usiku wa jumamosi matememeko madogo yaliendelea kutikisa na kuleta hofu zaidi. Watu wa jiolojia wa Marekani ambao hufanyakazi ya kuangalia matetemeko duniani  wamesema kwamba kumekuwa na matetemeko madogo 15 ya magnitude 4.5 na mengine yalikuwa ya 6.6 na 5.1.
Katika nchi jirani China maeneo ya Tibet, majengo yameanguka na watu 12 wamekufa.
Moja ya maeneo ya kihistoria yaliyobomoka ni mnara wa Dharahara ambao pia unajulikana kama Bhimsen Tower umeporomoka.Mnara huo uliojengwa mwaka 1832, ulikuwa na urefu wa mita 60 sawa na futi 200 na ulikuwa unatumika kuangalia bonde la Kathmandu .
CNN imesema kwamba tetemeko hilo ni kubwa la kwanza kwa takribani mikaa 80. Mwaka 1934 Nepal ilipigwa na tetemeko la 8.1 na kuua zaidi ya watu 10,000.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts

Popular Posts

© Copyright Right Vision Blog | Designed By Code Nirvana
Back To Top