.jpg)
Wednesday, April 08, 2015 5:11 PM
Mhadhiri wa Chuo Cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere,Shadrack Mwakalila akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kozi ya uongozi na maadili ya chuo hicho ,Kushoto ni Mhadhiri Msasidizi wa Chuo Cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere,Amon Katunzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Rais Dk.Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kozi ya uongozi na maadili iliyoanzishwa na Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere itayofanyika Aprili 13.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,jijini Dar es Salaam,Mhadhiri w Chuo Kumbukumbu Cha Mwalimu Nyerere,Shadrack Mwakalila,amesema kozi hiyo watasoma kwa muda wa miezi mitatu na itakuwa endelevu.
Mwakalila amesema kozi hiy ni kujenga watu kuwa na maadili ya kutokana na jinsi alivyowajibika Mwalimu wakati wa uhai wake.
Amesema watu wajitokeze katika kusoma kozi hiyo ambayo itasaidia kuwa viongozi na wenye maadili kutokana na kozi hiyo iliyoandaliwa.


Post a Comment