


Watu
10 wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la
Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5
asubuhi ya leo.
Akizungumza
na East Africa Radio Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa
Tanga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari
dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha.
Kwa
mujibu wa Kamanda gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua
mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa
likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.
Baada
ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na
kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngolika lililokuwa likitokea Dar
es salaam kwenda Arusha.
Aidha kamanda huyo
amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano wakiwemo
dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake
watano wakiwemo watoto wawili.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema pepon


Post a Comment