Msanii
wa muziki wa bongo flava Msami amemkana kiaina mrembo na
msanii wa bongo movie Irene Uwoya akitia ugumu kukubali moja
kwa moja kama ni wapenzi.
Msami
katika mahojiano na Mamu Africa Blog alikuwa mgumu kukubali
moja kwa moja kama wana mahusiano ya mapenzi na Uwoya
akisisitiza kuwa mrembo huyo ni zaidi ya rafiki.
Akaenda
mbali zaidi akisema mara kadhaa amekuwa analala na Uwoya
kitanda kimoja hata siku mbili mpaka tatu lakini wanalala
mzungu wa nne.
"Unajua
Uwoya ni best friend wangu sana sana,wakati mwingine
nakwenda kwake tunapiga stori mpaka usiku,tunaangusha pamoja
hata siku mbili tatu kitanda kimoja lakini huwa tunalala
mzungu wa nne tu" alisema Msami.
Msami
aliendelea kuzunguka kuukubali akitumia neno kwa mfano kama ni
wapenzi na Uwoya kukutana kwao ni baada ya kazi zao kwakuwa
kila mmoja ana majukumu yake ya kikazi.
"Unajua
kwa mfano tuna imagine kuwa Uwoya ni mpenzi wangu,mara nyingi
tunakutana baada ya mihangaiko yetu ya kila siku.
Baada ya danadana za hapa na pale na kubanwa hatimaye Msami akakiri kuwa kweli anatoka kimapenzi na Uwoya.
Aidha
Msami amesema anashangaa watu wanaosema kuwa Uwoya anatoka na
Serengeti boy wakati hawaujui ukweli wa jambo hilo,kwakuwa yeye
ana umri mkubwa zaidi ya mrembo huyo.
Amesema amemzidi Uwoya kwa kuzaliwa kwa miezi kadhaa kwahiyo yeye sio Serengeti boy kwakuwa ni mkubwa kwake.
"Nawashangaa
watu wanasema eti Uwoya anatoka na Serengeti Boy yaani hata
ukweli hawaujui mimi ni mkubwa nimemzidi miezi kadhaa
wanasemaje eti ni Serengeti Boy waache hizo" Msami alisema.



Post a Comment