Jamaa mmoja ambaye jina lake halikupatikana anayesadikika kuwa ni
tapeli mchana huu kashushiwa kipondo na wananchi wenye hasira kali mara
baada ya yeye na wenzake kufanikiwa kumtapeli mfanyabiashara mmoja
maarufu jijini hapa wakifanya biashara naye na kumlipa makaratasi na si
fedha halali yaani dola za kimarekani kama makubaliano yalivyokuwa.
Akiwa na wenzake huku wakitumia usafiri wa gari aina ya Noah yanye
namba za usajili za Uganda (bahati mbaya hazikunukuliwa) Tapeli hilo
(pichani) mara baada ya kukamilisha kufanya biashara na tajiri huyo
kuwapatia mali, Matapeli hayo yaliondoka eneo la biashara huku
wakimwacha tapeli mwenzao aliyepichani hatua chache toka eneo la tukio
ili asome harakati za mfanya biashara huyo pindi atakapostukia kuwa
kapewa makaratasi ya kimazingaombwe na si za madolali kama halali ya
malipo.
Waliposepa wazeeya, yule Mfanyabiashara
maarufu akagutukia mchezo ingawa alikuwa kisha chelewa kwani matapeli
wengine walikwisha timua eneo la unoko.
Angaza huku
na kule ...mara nkabaaaaa jicho likamnasa mmoja aliyewaona nao...
mfanyabiashara akakusanya washirika wenzake ... mara tip ... tapeli
aliyekuwa akichungulia msala akanaswa na kuanza kuchezeshwa kichapo.
 |
| Ni daftari lililokatwa kiufundi saizi ya dola za kimarekani |
Wengi wafanyabiashara hususani wa samaki na wavuvi wamekwisha lizwa
na matapeli hao jijini hapa wakibamizwa na biashara za dhahabu feki,
almasi feki na mitindo mingine ya kubadilisha fedha za madafu kwa dola
za Kimarekani.
Makaratasi hayo yalikuwa yameviringishwa vizuri kwenye karatasi ya kaki na kuwekewa raba bendi mtuno wake mithili ya fedha.
Mashambulizi huku jamaa huyo akitafuta njia kujinasua mikononi mwa wenye hasira.
Akikimbilia kwenye gari la maafande waliokuwa na safari zao kuelekea lindoni..
Dushwaaaa... akajitumbukiza kujisalimisha....
Vuta pumzi
Tuesday, April 7, 2015
Post a Comment