Featured
Loading...

Kwa matukio haya ya Songea , ACT-Wazalendo ina kazi kubwa

Leo umefanyika mkutano wa ACT-Wazalendo huku Songea ambapo ulihudhuriwa na watu wengi sana ambao kimsingi watu hao wengi wao ni wanachama wa CHADEMA.

Katika mkutano huo wengi waliohudhuria walihudhuria wakiwa na lengo la kusikiliza na kupima sera za chama hicho lakini cha ajabu hadi mwisho wa mkutano wananchi wamekiri kwamba CHADEMA ni chama imara huwezi kukifananisha na
ACT-Wazalendo .

Matukio haya mawili yaliyotokea mwishoni mwa mkutano huo ni ishara kwamba bado watu hawajaridhika na sera za chama hicho.

Tukio la kwanza mwishoni mwa mkutano Zitto aliwataka wananchi wote wanyoshe mikono juu lakini bahati mbaya sana umati mkubwa hawakunyosha mikono.

Lakini tukio la pili ambalo lilitokea nalo mwishoni ni pale alipowataka wahudhuriaji kucheza kwa pamoja wimbo wa ACT uzalendo lakini hakuna hata mmoja aliyecheza zaidi ya Zitto na Afande Sele pamoja na meza kuu.

Lakini mazungumzo ya watu katika vijiwe vingi vya vijana jioni hii ni kwamba moja wanalaumu uongozi huo wa
ACT-Wazalendo sababu hasa ya kumpa mtu mwenyekiti wa ACT-Wazalendo mkoa mtu ambaye amewahi kuwa kiongozi karibu vyama vyote vya siasa hapa nchini.

Mwenyekiti huyo wa mkoa wa
ACT-Wazalendo amewahi kuwa NCCR Mageuzi, CHADEMA, CUF lakini kote huko alikorofishana na wenzake na wakamfukuza na si hivyo tu jana ulitokea ugomvi mkubwa na vijana wa pikipiki wakati wanapewa fedha za mafuta kwa ajiri ya kumpokea Zitto leo wakidai kwamba mwenyekiti huyo anataka kubana fedha.

Kimsingi
ACT-Wazalendo itawachukua miongo zaidi ya miwili ili mfanane na CHADEMA

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts

Popular Posts

© Copyright Right Vision Blog | Designed By Code Nirvana
Back To Top