Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Licha ya Diamond
kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati
waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito
lakini safari hii Diamond amesema ndiyo basi tena!
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo
makini kilicho karibu na staa huyo, mara kwa mara Diamond amekuwa
akijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake na kusisitiza kwamba pamoja na
kuwa maisha ya sasa huendeshwa kwa msingi wa fedha lakini hata kama
‘atafulia’ kiasi gani, ni bora afe maskini kuliko kurudiana na Wema.
“Diamond amekuwa akisema
kila wakati kwa msisitizo kuwa kutokana na matatizo aliyokumbana nayo
katika uhusiano wake kwa Wema, ni vigumu sana kurudiana naye wala kuwaza
kama ipo siku anaweza kuwa naye, maana hakuna tena jambo geni
asilolijua kwake,” kilisema chanzo hicho na kufunguka zaidi:
“Kama hiyo haitoshi,
Diamond anasema anaposema haoni kitu kipya kwa Wema anamaanisha ndiyo
maana utaona leo hakuna hata siku moja ambayo amewahi kuwaza kurudiana
naye hata kama atatumia ushawishi wa fedha kwa kumpelekea makontena ya
fedha, hawezi kukubali anasema bora afe maskini kuliko kushea kitanda
kimoja na Wema.”
DIAMOND ATHIBITISHA
Baada ya madai hayo,
Risasi Jumamosi lilifanya jitihada za kukutana na Diamond uso kwa uso
ambaye alithibitisha taarifa ambazo zilielezwa na mtu wake wa karibu:
“Umeambiwa na nani hayo?
Sipendi kuongelea sana hivi vitu lakini huo uliousikia ndiyo ukweli.
Kwa sasa nawaza maisha yangu na mpenzi wangu Zari baada ya kupitia
majaribu mengi kimapenzi enzi hizo.
“Huenda wengi wasiamini
ninayosema lakini nafsi yangu haijawahi kuniongoza kukumbuka ya nyuma
tena kama ilivyowahi kutokea awali.
“Wengi wamekuwa
wakiniuliza swali kama hili lakini sikupenda kujibu kwa kuwa nilihisi
litaleta tafrani kwa mashabiki wangu, sioni sababu ya kuendelea kuulizwa
kwenye media hivyo ukweli ni kwamba siwezi kurudi nyuma tena,” alisema
Diamond.


Post a Comment