Featured
Loading...

Diamond: Zari kaniweka kwenye kiganja

zarinahMSANII wa Bongo Fleva, Nassib Abdul (Diamond Platnumz), amesema ujauzito aliobeba Zarina Hassan ‘Zari’ anaona kama amewekwa kwenye kiganja cha mchumba wake huyo.
Diamond alisema licha ya kutokuwa na fikra ya kuwa na maisha ya kujenga familia na msichana huyo wa Uganda, ila ujauzito alionao unaotarajiwa kumletea mtoto umekuwa chachu kubwa ya kuongeza mapenzi kwa Zari.
“Sikutegemea kuwa na Zari, lakini kwa hali aliyonayo sasa ya ujauzito ni kama ameniweka kiganjani na sasa ninachoomba mtoto azaliwe salama na awe na akili nyingi,’’ alisema Diamond.
Diamond aliongeza kwamba wasichana wengi aliowahi kuwa na uhusiano nao walikosa vitu vya kufanana naye.
“Niliokuwa nao nadhani kulikuwa na vitu ambavyo havikukamilika, ndiyo maana hatukuwa tukiishi kwa muda mrefu na kuanzisha maisha kama haya na Zari,’’ alisema Diamond.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts

Popular Posts

© Copyright Right Vision Blog | Designed By Code Nirvana
Back To Top